Waziri Mkuu Majaliwa azungumza na wanafunzi akielekea Ruangwa

 

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akizungumza na wanafunzi wa Shule ya Msingi ya Ndanda iliyopo Wilaya ya Masasi na Shule ya Msingi Nachingwea iliyopo Wilaya ya Nachingwea.

Wanafunzi hao wako wilayani Nachingwea kwa ajili ya ziara ya kitaaluma ikihusisha ufanyaji wa mitihani ya kujipima ya ujirani mwema.

Aidha, wanafunzi hao walikuwa uwanja wa ndege wa Nachingwea kwa ajili ya Kujifunza majukumu ya uwanja wa ndege.

Mheshimiwa Majaliwa amewasili Wilayani Nachingwea akielekea Ruangwa ambapo atakuwa mgeni Rasmi katika harambee ya Kanisa Katoliki jimbo la Lindi kwa ajili ya Maandalizi ya Jubilei na ujenzi wa kanisa jipya la jimbo katoliki Lindi. Harambee hiyo inafanyika leo Julai 27, 2024 wilayani Ruangwa.



Chapisha Maoni

0 Maoni