Uhamasishaji kura kwa Serengeti watinga Chuo cha Mweka

 

Timu TANAPA imetembelea chuo cha usimamizi wa wanyamapori Mweka leo tarehe 25.07.2024 kwa lengo la kuhamasisha zoezi la upigaji wa kura Hifadhi ya Taifa Serengeti na Mlima Kilimanjaro zinazowania tuzo za World Travel Awards 2024.

Mlima Kilimanjaro unawania tuzo katika kipengele cha kivutio Bora cha Utalii barani Afrika kwa mwaka 2024 (Africa’s Leading Tourist Attraction 2024) wakati Serengeti ikiwania kipengele cha Hifadhi bora barani Afrika kwa mwaka 2024 (Africa’s Leading National Park 2024).


Chapisha Maoni

0 Maoni