Aliyekuwa rais wa Marekani Barack Obama, amemuidhinisha Makamu wa Rais wa Marekani Bi. Kamala Harris kuwa mgombea urais kwa chama cha Democratic na kumaliza minong’ono endapo angemuunga mkono.
Obama na mkewe Michelle Obama, wamesema katika taarifa yao
wanaimani Bi. Harris ana maono, sifa na nguvu zinazohitajika na Marekani kwa
wakati huu muhimu.
Ilielezwa kuwa Obama ni miongoni mwa watu 100 mashuhuri wa Democratic, ambao Bi. Harris aliongea nao baada ya Rais Joe Biden kutangaza kujitoa kwenye mbio za urais siku ya jumapili.
0 Maoni