Tusimamie malezi yenye maadili kwa vijana- Dk. Mwinyi

 

RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk. Hussein Ali Mwinyi amewahimiza Wazazi na Walezi kuhakikisha wanasimamia malezi bora yenye maadili kwa watoto na  vijana.

Alhaj Dk. Mwinyi aliyasema hayo leo Julai 26 , 2024 alipojumuika na Waumini wa Dini ya Kiislam katika ibada ya sala ya Ijumaa  msikiti wa Sheikh Sharaan Meli nne Unguja.

Aidha Dk.Mwinyi ameleeza kuwa ni wajibu wa kila mmoja kuhakikisha anasimamia malezi ya watoto na vijana kutokana kwa kuwa dunia imebadilika na sasa ni wakati wa utandawazi, hujifunza mengi kupitia mitandao ya kijamii. 

Rais Dk. Mwinyi amewataka Wazazi na walezi kuhakikisha wanawafundisha watoto na vijana elimu ya Dini ili kuwa taifa lenye raia wema na hofu ya Mungu.

Kwa upande mwingine Rais Dk. Mwinyi amehimiza kuendelea kuiombea nchi kudumisha amani, utulivu, umoja na mshikamano ili kuzidi kupiga hatua ya maendeleo.




Chapisha Maoni

0 Maoni