Mashambulizi ya moto mtandao wa reli yaikumba Ufaransa

 

Matukio ya mfululizo ya mashambulizi ya moto yameukumba mtandao wa reli ya mwendokasi nchini Ufaransa, saa chache kabla ya ufunguzi wa michuano ya Olimpiki Jijini Paris.

Kampuni ya Reli ya SNCF imesema ni mashambulizi makubwa yaliyolenga kudumaza mtandao, huku Waziri wa Uchukuzi wa Ufaransa akilaani mashambulizi hayo ya kuratibiwa.

Kutokana na matukio hayo abiria wapatao 800,000 wameathiriwa na kutatizwa kwa usafiri wa treni hali inayotarajiwa kuendelea hadi mwishoni mwa wiki.

Chapisha Maoni

0 Maoni