Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo
Dkt. Suleiman Selela akimkabidhi tiketi ya ndege nahodha wa timu ya Taifa ya
riadha Alphone Felix Simbu katika hafla ya
wachezaji na maofisa wa timu hiyo itakayoshiriki katika Michezo ya
Olimpiki ya Majira ya joto inayoanza
Ijumaa ijayo Julai 26 hadi Jumapili Agosti 11, 2024 jijini Paris na miji
mingine 16 nchini Ufaransa
Katika mashindano hayo ya 33 ya Olimpiki, kikosi cha
Tanzania kitakuwa na nahodha na mkimbiaji Alphonce Felix Simbu, pamoja na
mkimbiaji mwenzie Gabriel Geay ambao watashiriki katika mbio za Marathon
kwa wanaume.
Wengine katika msfara huo ni Jackline Juma Sakilu na
Magdalena Crispin Shauri, ambao watashiriki michuano ya Marathon kwa
wanawake.
Kikosi hicho pia kina waogeleaji wawili, Sophia Anisa Latiff
atakayechuana mita 50 freestyle, kategoria ya wanawake na Collins Phillip
Saliboko atakayecheza mita 100 freestyle kwa wanaume.
Mwanamichezo Andrew Thomas Mlugu, atayeshiriki katika
mashindano ya mchezo wa Judo, tayari yuko Paris akiwa katika kambi
maalumu ya mchezo huo.
Timu hiyo itaambatana na makocha watatu wa fani hizo tatu za
michezo, daktari wa timu, Mwambata wa Habari pamoja na maafisa wawili
kutoka TOC.
Zaidi ya wanamichezo 10,500 kutoka mataifa 206 wanatarajiwa
kushiriki katika matukio 329 na fani 45 tofauti za michezo. Kwa mara ya kwanza
kila jinsia itawakilishwa na wanamichezo 5,250.
0 Maoni