Tarehe 21 Julai ni siku mbaya kwa January Makamba?

 

Tarehe 21/7 unaweza kusema ni siku mbaya katika maisha ya aliyekuwa Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki January Makamba.

January Makamba jana tarehe 21/07/2024 uteuzi wake ulitenguliwa na Rais Samia Suluhu Hassan na nafasi yake kuchukuliwa na Balozi Mahmoud Thabit Kombo.

Lakini historia pia inatueleza tarehe 21/07/2019 aliyekuwa Rais Hayati Dk. John Magufuli pia alitengua uteuzi wa January Makamba alipofanya mabadiliko madogo ya baraza la mawaziri.

Mwaka 2019 January aliyekuwa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira aliondolewa na nafasi yake kuchukua George Boniface Simbachawene.

Kwa matukio hayo mawili ya kutenguliwa uteuzi wa uwaziri kwa January Makamba kufanyika tarehe na mwezi unaofanana unaweza kusema kwamba tarehe 21/07 ni siku mbaya kwa January Makamba.

Chapisha Maoni

0 Maoni