Watumishi wa Wakala ya Barabara Tanzania (TANROADS) mkoa wa
Dar es Salaam jana wametoa msaada wa mahitaji muhimu kwa binadamu katika kituo
cha Furaha na Amani cha Mtakatifu Thereza cha Mburahati jijini Dar es Salaam.
Akiongoza watumishi hao Meneja wa Mkoa huo, Mhandisi John
Mkumbo amesema mahitaji hayo ya vitu mbalimbali vyenye thamani ya shilingi
milioni mbili na elfu thelasini (2,030,000) yamewasilishwa ikiwa ni maadhimisho
ya Wiki ya Utumishi wa Umma inayofanyika kila mwaka nchini.
“Tunashukuru umetutembeleza kila mahali wanapoishi watoto wa
umri mbalimbali, wazee wasiojiwe na watoto wenye changamoto ya kimwili,
tumejionea mazingira yalivyo na hata uhitaji ninaamini kuna siku Mungu
atatuongoza tutakuja tena kutoa mahitaji yanayostahili,” amesema Mha. Mkumbo.
Naye Mhasibu Mwandamizi wa TANROADS Dar es Salaam, Bi. Neema
Mtengula amesema mbali na kuwa ni wajenzi wa barabara ili zipitike vizuri
lakini pia wamekuwa wakitoa misaada kwa jamii zenye uhitaji katika vituo vya
kulea wazee na watoto.
“Kwanza nakupongeza sana Sista kwa kazi ya utume unayofanya
ya kuwalea watoto ni nadra sana kwa mama ambaye hana mtoto akaweza kumlea mtoto
mwingine mwenye changamoto kwa mapenzi makubwa, nakupongeza sana kwa moyo wa
upendo ambao Mungu ameuweka ndani yako,” amesema Bi. Mtengule.
Kwa upande wake Sista, M. Gonzalo M,C amewashukuru
wafanyakazi hao wa TANROADS kwa majitoleo yao kwa ajili ya kituo hicho,
amewaomba wasiwachoke na wafike mara kwa mara kuwasaidia maana bado wanauhitaji
wa vitu mbalimbali kwa ajili ya watoto na wazee wanaolelewa hapo.
Sista amesema kuwa wanawapata watoto wa kuanzia umri wa
sifuri hadi miaka miatatu kutoka kwenye ofisi za Ustawi wa jamii wakiwa wengine
wametelekezwa na wazazi wao
hawajulikani, na wengine wanachangamoto za ulemavu wa viungo.
“Ninashukuru sana kwa moyo wenu mkuu mmeweza kutembelea nyumba yetu ya wahitaji mmejionea wenyewe wapo watoto wadogo sana jumla tuna watoto 34, wazee wasiojiweza 42 na watoto wenye changamoto mbalimbali za viungo wapo 22 bado tunahitaji misaada kutoka sehemu mbalimbali maana tuna watoto wadogo sana na wazee wengi hawajiwezi,” amesisitiza Sista Gonzalo.
0 Maoni