Taasisi ya Utafiti wa Misitu Tanzania (TAFORI) imewasisitiza
Watanzania kuwekeza katika misitu na kushiriki katika ufugaji nyuki kwa
kuzingatia njia sahihi zilizofanyiwa utafiti ili wapate tija katika rasilimali
za misitu zilizopo nchini.
Wito huo umetolewa na Mkurugenzi wa Utafiti wa Matumizi ya
Misitu Dkt. Chelestino Balama wakati akiongea na baadhi ya timu ya wataalamu wa
misitu na nyuki na waandishi wa habari
wa waliofika ofisi za TAFORI Mkoani
Morogoro na kutembelea baadhi ya tafiti zinazofanywa.
"Sisi kama taasisi ya TAFORI tunafanya tafiti ambazo ni
kwa ajili ya kuboresha vipato kwa jamii lakini pia kwa ajili ya kuboresha
uchumi wa nchi yetu .Mojawapo ni tafiti ya kuzalisha miti katika maeneo
mbalimbali ili kuwa na taarifa sahihi za miti anbayo inafaa kupandwa katika
eneo fulani ambapo Vijana wengi wamejikita huko na imekuwa ni sehemu ya ajira,"
alifafanua Bw. Balama.
"Lakini pia taasisi yetu imefanya utafiti ambao
unahusika na kuangalia rasilimali za misitu ikiwemo kuona ni namna gani
zinachangia kwenye kuokoa malighafi katika viwanda vya Misitu hapa nchini na
utafiti huu umekuwa na mchango mkubwa kwenye kuleta ajira kwa vijana, maana
wamejikita kuanzia kwenye mnyororo mzima.wa mazao ya misitu," alisema Bw.
Balama.
Afisa Mtafiti Mkuu kutoka TAFORI ambaye pia ni Kaimu
Mkurugenzi tafiti ya uzalishaji Misitu Dkt. Stephen Maduka ambaye amebainisha
uwepo wa bustani ya miti ya Utafiti ya TAFORI iliyopo Ofisini kwao kwa lengo
mahususi ya kufanya utafiti katika kunusuru miti ya asili isitoweke ikiwemo mti
wa Mkurungu, Msandali na Msekeseke inayovunwa kwa wingi kwa ajili ya biashara
ya utengenezaji samani, kuongeza thamani ya miti ya asili ya matunda.
Kwa upande wake Kaimu Mkurugenzi Mkurugenzi ya Utafiti wa
Ufugaji Nyuki TAFORI Bw. Allen Kazimoto amewataka Vijana na Wanawake kushiriki
kikamilifu katika Ufugaji Nyuki kwa kuzingatia ubora wa Mazao ya Nyuki
yanayokudhi soko la ndani na pia la Kimataifa ili waweze kupata tija katika
Ufugaji.
Aidha, Bw. Kazimoto ametoa rai kwa Watanzania kuacha kufanya shughuli za Kibinadamu pamoja na Matumizi ya viuatilifu vya mazao ya Kilimo yanayosababisha makundi ya Nyuki kupungua kila mara.
0 Maoni