Shirika la Reli Tanzania (TRC) leo imezindua rasmi safari yake ya treni ya umeme ya mwendokasi inayotumia reli ya SGR kutoka Dar es Salaam hadi Dodoma.
Safari hiyo ya treni ya mwendokasi ilibeba abiria wapatao 1000 ikiwa na mahebewa 14 kwa mujibu wa Mkurugezi Mkuu wa TRC Masanja Kadogosa.
Amesema kuwa safari hiyo ya kutoka Dar es Salaam hadi Dodoma iliyochukua muda wa saa 3 na dakika 25 imepokelewa kwa wingi na abiria kiasi ya kwamba baadhi ya abiria walikosa tiketi.
Juni 14, mwaka huu Shirika la Reli Tanzania (TRC) lilianza safari za treni ya kisasa (SGR) kutoka Dar es Salaam hadi Morogoro.
0 Maoni