Rais Samia kufanya ziara Morogoro, kuzindua SGR

 

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan anatarajia kuanza ziara ya kikazi ya siku tano Mkoa wa Morogoro kuanzia Agosti 02, 2024.

Taarifa iliyotolewa imesema katika ziara yake hiyo mbali na kuzindua miradi mbalimbali ya maendeleo pia Rais Samia atazungumza na wananchi wa mkoa huo.

Aidha, Rais Dkt. Samia anatarajiwa kufanya uzinduzi wa safari za treni ya kisasa ya SGR kutoka Dar es Salaam mpaka Dodoma Agosti 01, 2024.

Chapisha Maoni

0 Maoni