Rais Samia aagiza mtoto mlemavu awekewe mguu wa bandia

 

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan ametoa maagizo kwa Ofisi yake pamoja na Wizara ya Afya kuhakikisha mtoto mwanafunzi wa darasa la Tatu Shule ya Msingi Tunduma, Ebenezer Wile Mwakasyele (8) huyo anatengenezewa mguu wa bandia mara moja.

Mtoto huyo mlemavu alikuwa pembezoni mwa barabara wakati akimsikiliza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia alipokuwa akiwahutubia wananchi Tunduma Mkoani Songwe leo tarehe 18 Julai 2024.

Wakati huo huo Rais Dkt. Samia amegharamia kiasi cha shilingi milioni 8 kwa ajili ya matibabu ya mtoto Mkazi wa Mbozi Mkoa wa Songwe mwenye tatizo la moyo baada ya mzazi wa mtoto huyo kushindwa kupata fedha za matibabu.

Hayo yamejiri leo wakati Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan aliposimama eneo la Mlowo Wilaya ya Mbozi kwa lengo la kusalimiana na wananchi akiwa njiani kuelekea Uwanja wa Ndege Songwe akitokea Katavi na Rukwa.

Chapisha Maoni

0 Maoni