Mwalimu jela miaka 30 kwa kuruhusu kulawitiwa na denti

 

Mwalimu wa Shule ya Sekondari Naputa Wilaya ya Tandahimba mkoani Mtwara amehukumiwa kifungo cha miaka 30 jela kwa kosa la kuruhusu kuingiliwa kinyume na maumbile.

Kamanda wa Polisi wa mkoa wa Mtwara, Issa Suleiman amesema mwalimu huyo alijenga urafiki na mwanafunzi wa kidato cha nne kwa kuanza kumnunulia vitafunwa shuleni na kumtaka akamtembelee nyumbani.

Amesema mwanafunzi huyo alipoenda nyumbani kwa mwalimu alianza kumuonyesha video chafu kupitia simu janja na baadaye kumtaka amuingilie kinyume na maumbile na alopokataa,mwalimu alianza kumtishia

Kamanda Suleiman amesema baada ya vitisho hivyo mwanafunzi huyo alilazimika kutekeleza kitendo hicho pasipo ridhaa yake.

Chapisha Maoni

0 Maoni