Aliyekuwa RC wa Simuyu kizimbani kwa kulawiti

 

Aliyekuwa Mkuu wa Mkoa wa Simiyu Dkt. Yahaya Nawanda amepandishwa kizimbani katika Mahakama ya Mkoa wa Mwanza na kusomewa shtaka moja tu la kulawiti.

Dkt. Nawanda amepanda kizimbani leo, mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu wa Mahakama hiyo Erick Marley na kusomewa shtaka hilo na waendesha mashataka wa Serikali, Magreth Mwaseba na Martha Mtiti.

Kwa mujibu wa Mwendesha Mashtaka Mwaseba, mshtakiwa Dkt. Nawanda alitenda kosa hilo kinyume na kifungu namba 154 (1) (a) cha Sheria ya Kanuni ya Adhanu sura ya 16.

Mshtakiwa alilikana shtaka hilo, ambapo upande wa mshataka uliieleza Mahakama kuwa upelelezi wa shauri hilo umekamilika, hivyo unaomba tarehe nyingine kwa ajili ya mshtakiwa kuanza kusomewa hoja za awali.

Wakli wa Dkt. Nawanda, Constantine Mutalemwa aliomba mteja wake kupatiwa dhamana, ambapo Hakimu Marley aliridhia kutolewa dhamana na mshtakiwa alitimiza masharti ya dhamana na kuachiwa kwa dhamana hadi Juali 16, 2024 kesi hiyo itakapoanza kusikilizwa.

Chapisha Maoni

0 Maoni