Waziri Mkuu Kassim Majaliwa leo Julai 15, 2024 amekagua na
kuzindua mitambo na vifaa vipya vya kurushia matangazo vya kampuni ya Azam
Media Limited.
Vifaa hivyo ni pamoja na Magari ya kisasa ya kurushia
matangazo (OB Van), kamera za kisasa pamoja na mfumo wa kusaidia maamuzi
viwanjani (VAR).
Vifaa hivyo vilivyogharimu shilingi bilioni tano vitatumika
katika kurushia matangazo ya mpira wa miguu wa ligi Kuu Tanzania bara na
Zanzibar pamoja michezo mingine.
Akizungumza na wafanyakazi wa Azam Media pamoja na wadau wa
michezo Mheshimiwa majaliwa amesema manunuzi ya vifaa hivyo ni mapinduzi
makubwa katika tasnia ya habari kwani kunaifanya Tanzania kuwa nchi ya kipekee
kuwa na vifaa vya kisasa vya aina yake katika ukanda wa Afrika Mashariki.
Mheshimiwa Majaliwa pia ameshuhudia uzinduzi wa chaneli mpya ya Azam 4 HD ambayo itatumika kurusha Ligi Kuu ya Ufaransa (Legue 1) na Ligi Kuu ya Ujerumani (Bundesliga).
0 Maoni