Gari la watalii lapata ajali Serengeti na kuua Mtalii Mchina

 

Mtalii mmoja raia wa China amefariki dunia baada ya gari la watalii lenye namba za usajili T603 DCL la Kampuni ya Yonda Afrika kupata ajali katika Hifadhi ya Taifa ya Serengeti.

Taarifa iliyotolewa na Shirika la Hifadhi ya Taifa (TANAPA) imesema ajali hiyo iliyotokea jana majira ya saa 10 jioni kilomita moja kutoka Lobo Wildlife Lodge imejeruhi pia watalii wengine sita raia wa China.

Taarifa hiyo iliyotolewa Afisa Uhifadhi Mkuu TANAPA Catherine Mbena imesema mwili wa marehemu umehifadhiwa katika hospitali ya Mugumu na majeruhi sita wanaendelea kupata matibabu katika hospitali hiyo.

Uchunguzi unaendelea kwa kushirikiana na mamlaka zingine ili kubaini chanzo cha ajali hiyo, imemalizia taarifa hiyo.

Chapisha Maoni

0 Maoni