TUCTA yaipongeza Serikali kwa kuongeza malipo ya mkupuo

 

Shirikisho la Vyama vya Wafanyakazi Tanzania (TUCTA) limeipongeza Serikali kwa kuongeza kiwango cha malipo ya mkupuo ya pensheni kwa wastaafu kutoka asilimia 33 mpaka 40 kwa wafanyakazi waliokuwa wanapokea asilimia 50 kabla ya mifuko kuunganishwa na asilimia 35 kwa watumishi ambao walikua wakipokea asilimia 25 kabla mifuko hiyo kuunganishwa.

Pongezi hizo zimetolewa na Rais wa TUCTA, Tumaini Peter Nyamhokya katika mkutano na waandishi wa habari uliofanyika jana mkoani Morogoro.

“Kipekee sana tunampongeza Rais Samia Suluhu Hassan kwa kusikia kilio hiki cha muda mrefu cha watumishi, ameonesha mapenzi yake kwetu. Ni matumaini yetu kwamba baada ya mwanzo huu mzuri basi hali itakapokaa sawa asilimia hizi zitaongezeka kufikia 50.

Amesema Nyamhokya wakati wa Kikao cha Kamati ya Utendaji cha Shirikisho hilo na kuongeza kuwa nyongeza hizo zitapunguza kwa kiasi kikubwa malalamiko ya wafanyakazi.

Na. Moses Kwindi- Morogoro

Chapisha Maoni

0 Maoni