Waziri wa Maliasili na Utalii Mhe. Angellah Kairuki (Mb) ameipongeza Taasisi
ya Utafiti wa
Wanyamapori Tanzania (TAWIRI)
kwa kuthamini umuhimu wa wadudu
katika sekta ya uhifadhi na
kuanzisha maabara maalumu ya kuwahifadhi wadudu wote wanaopatikana hapa nchini na nchi nyingine.
Waziri Kairuki ametoa
pongezi hizo katika maonyesho ya Karibu
Kili Fair 2024 ambayo
yamehitimishwa leo 9 Juni, 2024 jijini
Arusha ambapo pia ameelekeza taasisi hiyo kuona fursa za utalii katika swala
zima la wadudu.
Aidha, ikiwa tafiti chache za wadudu zimefanyika atika nchi
nyingi zinazoendelea huku kipaumbele
kikitolewa kwa wanyamapori wakubwa , TAWIRI inajivunia kuwa na Maabara hii ya wadudu ambayo ni kituo muhimu na
sahihi kwa ajili ya kuhifadhi makundi mbalimbali ya wadudu yanayofanyiwa
utafiti .
Akizungumza na Mwanahabari
wetu, Mtafiti wa Wadudu kutoka
TAWIRI Neema Kilimba amesema kupitia
maabara ya Wadudu, TAWIRI kwa
kushirikiana na wadau wengine
inakamilisha Kanzidata ya makundi mbalimbali ya wadudu wanaopatikana Tanzania
na nchi nyingine.
Vilevile kupitia
maabara hii, TAWIRI inaandaa orodha ya makundi mbalimbali ya wadudu na
mtawanyiko wao nchini (atlas of insects) wakiwemo nyuki, mbawakawa
wanaoviringisha vinyesi (dung beetles), wadudu wa maji baridi (aquatic insects
of fresh water) na mbawakawa wanaoishi ardhini (carabidae - beetles).
Mtafiti Kilimba
amebainisha, uwepo wa kanzidata
ya makundi mbalimbali ya wadudu utasaidia
kutambua aina mbalimbali za wadudu tulizonazo pamoja na makazi na
mtawanyiko wao hivyo kuchochea uhifadhi wa bioanuwai hii muhimu, kutoa elimu na msingi wa takwimu kwa watafiti na wanafunzi mbalimbali.
"Uwepo maabara ya wadudu imeamsha ari ya watafiti na
wanafunzi kusoma na kufanya tafiti za wadudu ambao wanamchango mkubwa katika
maisha ya binadamu, wanyama na mimea," amesema Mtafiti Kilimba.
Ameongeza Wadudu
wanachangia uchavushaji wa mimea kwa zaidi ya asilimia 80%, uozeshaji na umeng'enyaji wa taka hususani vinyesi na usafishaji wa
mazingira(decomposition), uoteshaji wa mbegu mbalimbali, uongezaji mbolea
kwenye udongo ( soil fertilization ), kuwezesha makazi ya wanyama wengine. Pia
Wadudu ni chakula kwa wanyama wengine na sehemu muhimu kwenye mzunguko wa
chakula (food chain).
Vilevile wadudu wanatumika kama viashiria vya afya ya mifumo
ya kiikolojia. Wadudu wanachangia kwa asilimia kubwa kuongeza kipato kwa jamii
kwa kuuza wadudu wenyewe kama chakula au bidhaa zitokanazo na wadudu.
TAWIRI inawakaribisha wadau mbalimbali kujifunza kuhusu wadudu na ufugaji bora wa nyuki. Pia tunatoa elimu ya kisayansi (Scientific talks) kuhusu wadudu na wanyamapori wengine kwa wadau wa utalii, wanafunzi na watafiti sambamba na kutoa ushauri (consultancy) ya uwekezaji kwenye sekta ya utalii.
0 Maoni