Hafla ya Utoaji wa Tuzo za Wanamichezo Bora wa Mwaka 2024

 

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akipokea tuzo ya heshima katika sekta ya michezo kutoka kwa Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo Dkt. Damas Ndumbaro, kwenye ukumbi wa The Super Dome Masaki Jijini Dar es Salaam Juni 09, 2024. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akizungumza kwenye Hafla ya Utoaji wa Tuzo za Pili (2) za Baraza la Michezo la Taifa kwa Wanamichezo Bora wa Mwaka 2024, katika ukumbi wa The Super Dome Masaki Jijini Dar es Salaam Juni 09, 2024. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akimpa tuzo ya Mwanamichezo Bora wa Kike Bondia Grace Mwakamele wakati wa Hafla ya Utoaji wa Tuzo za Pili (2) za Baraza la Michezo la Taifa kwa Wanamichezo Bora wa Mwaka 2024, kwenye ukumbi wa The Super Dome Masaki Jijini Dar es Salaam Juni 09, 2024. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akimpa tuzo ya Mwanamichezo Bora wa Kiume Bondia Yusuf Lucas  Changarawe wakati wa Hafla ya Utoaji wa Tuzo za Pili (2) za Baraza la Michezo la Taifa kwa Wanamichezo Bora wa Mwaka 2024, kwenye ukumbi wa The Super Dome Masaki Jijini Dar es Salaam Juni 09, 2024. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

Chapisha Maoni

0 Maoni