TANAPA yatumia zaidi ya milioni 144 kujenga ujirani mwema Bunda

 

Wizara ya Maliasili na Utalii Kupitia Shirika la Hifadhi za Taifa (TANAPA) katika kipindi cha Mwaka 2020/2021 na Mwaka 2022/2023 ilitumia jumla ya Shilingi 144,268,404 kujenga nyumba ya Mganga na Nesi (mbili kwa moja) pamoja na kutengeneza samani kwa ajili ya Kituo cha Afya Hunyari, Wilayani Bunda Mkoani Mara. 

Haya yamebainishwa na Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii Mhe. Dunstan Kitandula(Mb) alipokuwa akijibu swali la Mhe. Boniface Mwita Getere(Mb) aliyetaka kujua TANAPA itamalizia lini  jengo la upasuaji katika Kituo cha Afya Hunyari wilayani Bunda. 

Mhe. Kitandula aliongeza kuwa Wizara ya Maliasili na Utalii kupitia TANAPA imeweka utaratibu wa kufadhili miradi ya ujirani mwema kwa maeneo yanayozunguka Hifadhi za Taifa. 

Vile vile, ili kuendelea kunufaika na miradi ya ujirani mwema ambayo ni sehemu ya manufaa ya shughuli za Uhifadhi na Utalii, “Natoa rai kwa wananchi wa Kijiji cha Hunyari Wilayani Bunda kutumia utaratibu uliowekwa na TANAPA katika kufadhili miradi ya ujirani mwema kwa kutuma maombi rasmi kuhusiana na umaliziaji wa jengo hilo la upasuaji,” alisema Mhe. Kitandula.

Na. Anangisye Mwateba-Bungeni Dodoma 

Chapisha Maoni

0 Maoni