Rais Samia amlilia mtoto mwenye Ualbino aliyeuawa

 

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan ameoneshwa kuguswa na kusikitishwa mno na tukio ka kifo cha mtoto mwenye Ualbino Asimwe Novath (2), ambaye alitekwa na kuuawa.

Rais Samia ameonyesha kuumizwa na tukio hilo na kulitolea kauli yake leo leo Juni 18,2024 Jijini Dar es Salaam, wakati akifungua Kongamano la Pili la Maendeleo ya Sekta ya Habari, lililofanyika kwenye ukumbi wa Mlimani City Jijini Dar Salaam.

Mwili wa mtoto Asimwe aliyetekwa kwa zaidi ya wiki mbili ulepatikana jana Juni 17, ukiwa umefungwa kwenye mfuko (sandarusi) huku ukiwa hauna baadhi ya viungo kama ulimi na mikono yote miwili.

Tukio la kutekwa kwa mtoto huyolilitokea Mei 30, 2024 akiwa na mama yake mzazi huko nyumbani kwao kitongoji cha Mbale, kijiji cha Bulamula, kata ya Kamachumu, wilaya ya Muleba mkoani Kagera, ambapo walivamiwa na watu wasiojulikana majira ya saa 2:30 usiku wakamkaba mama yake na kisha kuondoka na mtoto pekee.

Chapisha Maoni

0 Maoni