Polisi Mbeya wamshikilia dereva aliyesababisha ajali iliyoua watu 13

 

Jeshi  la Polisi Mkoa  wa  Mbeya linamshikilia  Dereva  wa Sacania  namba T979CVV na tela namna T758 BEU, Ross  Mwaikambo  (40), kwa kusababisha ajali iliyoua watu 13 katika eneo la Mbembela, Kata ya Iyunga  Jijini Mbeya katika barabara  kuu ya  Mbeya- Tunduma.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mbeya SACP Benjamin Kuzaga, amesema dereva huyo ambaye anaendelea na matibabu katika Hospitali ya Rufaa Kanda ya Mbeya akiwa chini ya ulinzi, alikuwa akitokea eneo la Shamwengo akiwa amepakia kokoto.

Amesema kwamba dereva huyo, aliligongana  na  gari  namba  T.167 DLF Toyota Coaster iliyokuwa ikiendeshwa  na dereva asiyefahamika  kisha  kugongana  na  Gari namba  T.120   DER  Toyota   Harrier  iliyokuwa ikiendeshwa  na Dokta Robert Francis Mtungi (48) Mkazi wa Isyesye.

Aidha,  Lori  hilo liliendelea  kugonga Guta namba  MC  660  BCR iliyokuwa ikiendeshwa na dereva asiyefahamika kisha kugonga  Pikipiki  namba  MC 889 CKX iliyokuwa ikiendeshwa na dereva asiyefahamika  na kusababisha  vifo  vya watu kumi na tatu (13) kati yao wanawake 5, wanaume 8 na majeruhi kumi na nane [18]  kati yao  wanawake  4  na wanaume  14  na uharibifu wa vyombo  vya moto.

Kamanda Kuziga amesema majeruhi wamepelekwa katika Hospitali ya Rufaa Mbeya kwa matibabu na miIli ya marehemu imepelekwa Hospitalini hapo kwa hifadhi na kusubiri k utambuliwa, huku akieleza kwamba chanzo cha ajali ni uzembe wa Dereva wa Gari namba T979CVV/T758 BEU kushindwa kulimudu gari kwenye mteremko.

Chapisha Maoni

0 Maoni