Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe.
Geophrey Pinda ametaka mradi wa ujenzi wa Chuo cha Ardhi Morogoro unaojumuisha
eneo mahali chuo kilipo na eneo la mlima Kola kuwekewa nguvu ili uweze
kukamilika kabla ya muda uliopangwa.
Mhe. Pinda ametoa kauli hiyo leo tarehe 29 Juni 2024 wakati
alipokwenda kukagua eneo la ujenzi wa mradi huo katika eneo la mlima Kola
mkoani Morogoro.
Mradi wa ujenzi wa Chuo cha Ardhi Morogoro unaojumisha
mahali chuo kilipo pamoja na eneo la Mlima Kola umeelezwa kuchukua miaka 20
mpaka kukamilika kwake mwaka 2043 na
utagharimu kiasi cga shilingi bilioni 70 ambapo
bilioni 64 zitawekezwa eneo la mlima Kola na bil 6 kwenye kampasi ya chuo
Kilakala.
Mradi huo unajumuisha Jengo la Utawala, Madarasa, Maktaba, Hosteli
za Wanafunzi, Kumbi kubwa za kufundishia, Zahanati, Migahawa pamoja na maeneo
ya kuabudia.
Kwa mujibu wa Kaimu Mkuu wa Idara ya Taaluma Pius Kafefa,
vyanzo vya mapato kwa ajili ya ujenzi wa mradi huo wa chuo cha ARIMO ni ada za wanafunzi, miradi mbalimbali ya
chuo kama vile ushauri wa kitaaluma, fedha kutoka serikalini pamoja na
maombi kutoka kwa wafadhili.
Naibu Waziri wa Ardhi Mhe. Pinda amesema, ni vyema mradi huo
ukawekewa nguvu ili uende kwa haraka kwa kuwa kuchukua muda mrefu kutafifisha
uharaka wa maendeleo ya chuo.
"Kujipa muda mrefu kukamilisha mradi wa chuo chenu
hakuko sawa kabisa na sisi tunataka mradi uishe haraka ili tuwe na matokeo ya
muda mfupi sambamba na waanzishaji mradi kuushuhudia," amesema Mhe. Pinda.
Ameutaka uongozi wa chuo cha ARIMO kuandika mapendekezo ya namna ya kukamilisha ujenzi wa mradi huo
kwa haraka ili wizara ya Ardhi Nyumba na
Maendeleo ya Makazi ione namna ya kusaidia ili uishe kabla ya muda wa miaka 20
uliopangwa.
Mwenyekiti wa Bodi ya Chuo cha Ardhi Morogoro Profesa Ernest Kahanga ameeleza kuwa, changamoto kubwa inayokikabili chuo ni upungufu wa walimu pamoja na miundombinu ambapo ameweka wazi kuwa, kama chuo hicho kingetatua changamoto hizo kingefanikiwa kudahili takriban wanafunzi 3000 na kukifanya chuo kusonga mbele kwa kasi na kuondokana na utegemezi.
Pinda ataka mradi ujenzi Chuo cha Ardhi Morogoro kuwekewa
nguvu

Na.Munir Shemweta- Morogoro
0 Maoni