Nyota wa soka Sofyan atembelea Mikumi

 

Kiungo wa Timu ya Manchester United ya Uingereza, Sofyan Amrabat ambaye pia huchezea kikosi cha kwanza cha Timu ya Taifa ya Morocco, amemaliza kutembelea Hifadhi ya Taifa ya Mikumi iliyopo Morogoro.

Sofyan akionesha kufurahia safari yake amepost akitania: “Tanzania, East Africa: Leo Simba wa Atlas (jina la utani la nchi yake) Amekutana na Simba Mwenyewe!” Awali Amrabat alikuwa ametembelea visiwa vya Karafuu Zanzibar.

Nyota kadhaa wa soka wa kimataifa wanatembelea kufanya shughuli za utalii duniani wakati huu wa mapumziko ambapo Tanzania inazidi kuwa moja ya maeneo pendwa.

Beki wa mabingwa wa soka wa Ufaransa PSG, Ashraf Hakimi naye yupo nchini Tanzania kwa mapumziko na ametembelea Hifadhi ya Taifa ya Ngorongoro.






Chapisha Maoni

0 Maoni