Mchungaji Peter Msigwa atimkia CCM

Aliyewahi kuwa Mbunge wa Jimbo la Iringa Mjini, kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Mchungaji Peter Msigwa amekihama chama hicho na kuhamia Chama cha Mapinduzi (CCM).

Mchungaji Msigwa amepokekewa CCM wakati wa Kikao cha Halmashauri Kuu ya Taifa ya Chama cha Mapinduzi (NEC) Jijini Dar es Salaam leo Juni 30, 2024 kilichoketi chini ya Mwenyekiti wa CCM Taifa, Rais Samia Suluhu Hassan

Mei 29 mwaka huu, Mchungaji Msingwa ambaye alishindwa kutetea uenyekiti wa kanda ya Nyasa, baada ya kushindwa na Joseph Mbilinyi, maarufu kama Sugu kwa tofauti ya kura mbili.


Chapisha Maoni

0 Maoni