Bilionea Yusuf Manji afariki dunia Marekani

 

Mfanyabiashara maarufu wa Tanzania Bilionea Yusuf Manji ambaye pia aliwahi kuwa Mwenyekiti na Mfadhili wa Klabu ya Yanga amefariki dunia.

Mtoto wa marehemu, Mahbub Manji, amethibitisha kuwa baba yake alifariki dunia majira ya saa 6 usiku wa kumakia leo, akiwa huko Florida nchini Marekani.

Manji amerejea nchini Tanzania kwa muda, baada ya Rais Samia Suluhu kuhimiza wafanyabiashara waliotoroka nchi kurejea na kuendelea na uwekezaji wao.

Manji alitorokea nje ya nchi mwaka wa 2018 baada ya Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu jijini Dar es Salaam kumuachia huru pamoja na wenzie watatu mwezi Septemba 2017 walipokuwa wakituhumiwa kwa makosa saba ya uhujumu uchumi.

Alituhumiwa pia kuhujumu usalama wa taifa kwa kukutwa na vitambaa vinavyotengeza sare za jeshi la wananchi wa Tanzania JWTZ vyenye thamani ya zaidi ya shilingi milioni 200 za Kitanzania.

Chapisha Maoni

0 Maoni