BRELA yamkabidhi Rais Samia Gawio la Shs Bilioni 18.9

 

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan leo tarehe 11 Juni, 2024, amepokea gawio la kiasi cha Shilingi 18,973,853,514.27 kutoka Wakala wa Usajili wa Biashara na Leseni (BRELA).

Hatua hiyo ni utekelezaji wa utoaji gawio kwa mujibu wa kifungu cha 10 cha Sheria ya Msajili wa Hazina Sura 370.

Hafla hiyo iliyofanyika Ikulu Jijini Dar es Salaam leo tarehe 11 Juni, 2024, imehudhuriwa na Dkt. Fred Msemwa Mjumbe wa Bodi ya Ushauri ya Wizara kwa BRELA na Bw. Godfrey Nyaisa Afisa Mtendaji Mkuu wa BRELA. 

Dkt. Fred Msemwa Mjumbe wa Bodi ya Ushauri ya Wizara kwa BRELA na Bw. Godfrey Nyaisa Afisa Mtendaji Mkuu wa BRELA, wakiwa kwenye picha ya pamoja na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan leo tarehe 11 Juni, 2024 wakati wa kukabidhi Gawio.

Chapisha Maoni

0 Maoni