Mradi wa BRT Posta kutoondoa Sanamu la Askari

 

Taarifa ya Kitengo cha Mawasiliano kwa Umma TANROADS

Tunapenda kufafanua taharuki iliyozuka kwenye mitandao ya kijamii kuhusu Askari Monument ya Dar es Salaam.

Ni kwamba ujenzi unaoendelea katika Mradi BRT Awamu ya Tatu hautaondoa wala kugusa SANAMU YA ASKARI iliyopo makutano ya Mtaa wa Azikiwe na Samora.

Hata hivyo, kutokana na ufinyu wa eneo la barabara katika makutano hayo, duara la bustani litapunguzwa bila kuathiri hadhi ya sanamu hiyo na usalama wa matumizi ya barabara.

Chapisha Maoni

0 Maoni