Waziri wa zamani wa fedha afariki dunia

 

Waziri wa zamani wa Fedha Mustafa Haidi Mkulo amefariki dunia leo katika hospitali ya Taifa Muhimbili alipokuwa amelazwa akipatiwa matibabu.

Taarifa iliyotolewa leo na mke wake Bi. Julie Mkulo, imesema shughuli za mazishi zitafanyika Msikiti wa Maamur na maziko yatafanyika kesho tarehe 5-05-2024 huko Kilosa Morogoro.

Wakati wa uhai wake Prof. Mkulo aliwahi kushika nyadhifa mbalimbali serikalini ikiwamo ya Mkurugenzi Mkuu wa NSSF.

Chapisha Maoni

0 Maoni