Filamu Mpya ya “Amazing Tanzania” Ft. Rais Samia, Dkt. Mwinyi Kuzinduliwa China

 

Filamu mpya ya kuitangaza Tanzania iitwayo “Amazing Tanzania” sasa itazinduliwa rasmi Mei 15 mwaka huu jijini Beijing, China ikiwa imewashirikisha Marais Dkt. Samia Suluhu Hassan na Dkt. Hussein Mwinyi kama waongozaji wakuu wa utalii, utamaduni na raslimali nyingine za nchi ikiwemo madini ya Tanzanite.

Hayo yamesemwa na Katibu Mkuu wa Wizara ya Maliasili na Utalii ambaye pia ni Mwenyekiti wa Kamati ya Rais ya Kuitangaza Tanzania, Dkt. Hassan Abbasi katika kipindi maalum na Wasafi FM mbashara kutokea Hifadhi ya Taifa ya Arusha kilichofanyika leo, katika moja ya mahali iliporekodiwa filamu hiyo.

Chapisha Maoni

0 Maoni