Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu
Hassan amepongezwa kwa kazi kubwa ya kutangaza utalii wa Tanzania duniani
katika kilele cha maadhimisho ya siku ya
Mei Mosi 2024 jijini Arusha.
Pongezi hizo zimetolewa leo, Mei 01, 2024 na Mkuu wa Mkoa wa
Arusha, Mhe Paul Makonda wakati akitoa salamu za mkoa wa Arusha.
Aidha, amesema tayari Mkoa wa Arusha kwa kushirikiana na
Wizara ya Maliasili na Utalii na Wizara ya Mipango na Uwekezaji wanakusudia
kujenga kituo cha Uwekezaji ambacho kitakuwa kikitoa huduma zote za sekt hiyo
kwa Watalii na wawekezaji wa sekta ya utalii.
"Ndugu mgeni rasmi naomba niseme, jana tumefanya kongamano
la Uwekezaji ha Arusha ambapo tumekubaliana kujenga One Stop Center kwa ajili
ya kutoa huduma zote za utalii mahali pamoja." Amefafanua, Mhe. Makonda
Kongamano hilo lilihudhuriwa na viongozi mbalimbali
wakiwemo, Waziri wa Maliasili na Utalii Mhe. Angellah Kairuki (Mb),Naibu Waziri
wa Wizara hiyo Mhe. Dunstan Kitandula, Katibu Mkuu Maliasili Dkt. Hassan
Abbasi, Katibu Mkuu Ofisi ya Rais, Mipango na Uwekezaji, Dkt. Tausi Mbaga Kida,
Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mhe. Paul Makonda, Viongozi Waandamizi wa Chama na
Serikali pamoja na Wadau wa Uhifadhi na Utalii wa jijini Arusha ambapo Mhe
Kitila Mkumbo, Waziri mwenye dhamana ya
Mipango na Uwekezaji alikuwa mgeni rasmi
Aidha, Watumishi wa
Wizara ya Maliasili na Utalii leo Mei
Mosi 2024 wameungana na Wafanyakazi Duniani kote kuadhimisha Siku hiyo hapa nchini Tanzania mkoani Dodoma na kwenye
Kilele cha Siku hiyo kitaifa Jijini
Arusha na Mgeni Rasmi wa Sherehe hizo ni Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe.
Dkt. Philip Isdor Mpango
Wizara ya Maliasili imefanikiwa kutangaza vivutio vya utalii
kupitia mashindano ya michezo ya Mei
Mosi 2024 yaliyoanza takribani wiki tatu
Iliyopita jijini Arusha na kufanikiwa
kunyakua vikombe mbalimbali.
Kauli mbiu ya siku hii ya Wafanyakazi Duniani kwa mwaka huu ni "Nyongeza ya Mishahara ni Msingi wa Mafao Bora na kinga Dhidi ya Hali Ngumu ya Maisha."
0 Maoni