Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dk.
Hussein Ali Mwinyi ameushukuru uongozi
wa Shirikisho la Soka Afrika(CAF) kwa
kuifanya Zanzibar kuwa mmoja ya waandaaji wa Mashindano ya African Football Championship mwaka huu.
Rais Dk. Mwinyi amesema hayo alipokutana na Rais wa
Shirikisho la Soka barani Afrika (CAF), Dk. Patrice Motsepe na ujumbe wake
waliofika Ikulu Zanzibar tarehe: 24 Mei 2024.
Aidha Rais Dk. Mwinyi amesema Zanzibar itaendeleza na kudumisha
uhusiano wake na CAF.
Rais Dk. Mwinyi amemueleza Dk. Motsepe kuwa Zanzibar
inahitaji msaada wa kuendeleza vipaji vya soka kuanzia ngazi za academy kwa
kushirikiana na CAF.
Rais wa CAF Dk.Motsepe leo atashuhudia mchezo wa kwanza wa fainali za Mashindano ya African Schools Football Championship yanayofanyika katika uwanja wa New Amaan Complex, Zanzibar.
Rais wa Shirikisho la Soka barani Afrika (CAF), Dk. Patrice Motsepe akimkabidhi mpira Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dk. Hussein Ali Mwinyi Ikulu Zanzibar tarehe: 24 Mei 2024.
0 Maoni