Chaguzi zisizo za haki chanzo cha migogoro Afrika- Kikwete

 

Rais Mstaafu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Jakaya Mrisho Kikwete, amesema Baraza la Amani na Usalama la Umoja wa Afrika ni Baraza ambalo limeonesha thamani yake katika kusimamia masuala ya amani na usalama katika bara Afrika hivyo ni suala la kujivunia.

Mhe. Kikwete amesema migogoro mingi Afrika inatokana na mapungufu ya kiutawala na demokrasia pamoja na kuwa na chaguzi ambazo si za haki.

Aidha, Mhe. Kikwete amesema Afrika itakuwa nchi ya amani zaidi iwapo itapambana na mapungufu ya kiutawala ambayo yanawanyima uhuru wananchi wa kukosa haki ya kufanya maamuzi.

Pamoja na mambo mengine Mhe. Kikwete amesema mapungufu hayo ndiyo yanayoleta ubaguzi katika jamii, ambapo jamii inagawanyika kindugu na kikabila hivyo kusababisha kutokuwa na mshikamano kama nchi na kuwa mwanzo wa migogoro.

Chapisha Maoni

0 Maoni