Wizara ya Maliasili yapania kuboresha hali ya wafanyakazi wake

 

Wizara ya Maliasili imepania kuendeleza halibora ya wafanyakazi wakati huu sekta hizo zikiendelea kuwa na nchango mkubwa katika uchumi wa nchi ikiwemo kuongoza kwa kuingiza fedha za kigeni kwa asilimia 25.

Hayo yameelezwa na Waziri wa Wizara hiyo Mhe. Angellah Kairuki wakati akifungua Kikao cha 31 cha Baraza la Wafanyakazi ambapo pia amewepongeza wafanyakazi wa Wizara hiyo na taasisi zake kwa utendaji na kufikia mafanikio mengi na kutaka wajitume zaidi hasa kuhifadhi na kuongeza zaidi idadi ya watalii nchini.

Awali Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Dkt. Hassan Abbasi na Mwenyekiti wa Baraza hilo alieleza mafanikio ya kiutendaji ikiwemo wizara hiyo kuwa ya kwanza kuhamia jengo jipya mji wa Serikali Dodoma, kununua magari mapya na vitendeakazi vingine na kuishukuru Serikali kwa kuongeza bajeti ya wizara hiyo katika mwaka ujao wa fedha.



Chapisha Maoni

0 Maoni