Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu
Hassan akipokea mfano wa Hundi ya Shilingi milioni 500 kwa ajili ya Mashindano
yanayohusu Timu za Taifa za Tanzania kutoka kwa Mfanyabiashara Said Naseer
Naseer kwa niaba ya Wafanyabiashara wenzake kutoka Zanzibar. Shughuli hii
imefanyika Ikulu Jijini Dar es Salaam tarehe 04 Aprili, 2024.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu
Hassan akimkabidhi Rais wa Shirikisho la mpira wa miguu Tanzania (TFF) Ndugu
Wallace Karia mfano wa Hundi ya Shilingi milioni 500 kwa ajili ya Mashindano
yanayohusu Timu za Taifa za Tanzania Ikulu Jijini Dar es Salaam. Fedha hizo
zimetolewa na Wafanyabiashara wa Zanzibar katika kumuunga mkono Rais Samia
kwenye michezo tarehe 04 Aprili, 2024. Kushoto ni Waziri Mkuu Kassim Majaliwa
akishuhudia.
0 Maoni