Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Mhe Albert Chalamila ametembelea na kukagua maeneo yaliyoathirika na mvua katika Wilaya ya
Kigamboni Jijini Dar es Salaam.
Akiwa katika ziara hiyo jana RC Chalamila amekagua miundombinu
mbalimbali ikiwemo daraja la kibada ambapo TANROAD wanaendelea na matengenezo
ya daraja hilo ili kurejesha mawasiliano.
Aidha, RC Chalamila amewatoa hofu wananchi kufuatia mvua
zinazoendelea kunyesha ambapo amesema Dar Es Salaam ni salama hakuna barabara
ambayo itaachwa bila kutengenezwa
barabara zote zitatengenezwa katika viwango tofauti "wananchi waendelee
kuchukua tahadhari ikiwemo kuhama mabondeni" Alisema RC Chalamila.
Vilevile Mhe Mkuu wa Mkoa ameelekeza kuanza kwa oparesheni
ya kuondoa vipenyo ili kuruhusu maji yapite ikiwemo kubomoa Kuta zinazuia maji
kupita.
Sambamba na hilo RC Chalamila amezitaka Halmashauri zote
katika Mkoa huo kutoa fedha ambazo ziliwekwa katika bajeti kwa ajili ya TARURA
ili Kuharakisha urekebishaji wa maeneo yote yaliyoharibiwa na mvua.
Mwisho RC Chalamila amezitaka TANROAD na TARURA kufanya kazi usiku na mchana katika nyakati hizi za mvua " Kabla ya usiku wa kesho April 24, 2024 barabara ziwe zinapitika.
0 Maoni