Mvua zasababisha vifo vya watu 15 ndani ya siku 7

 

Watu 15 wamepoteza maisha katika kipindi cha siku saba kutokana na kusombwa na maji kufuatia mvua zinazoendelea kunyesha katika maeneo mbalimbali ya nchi.

Msemaji wa Jeshi la Polisi Nchini David Misime amesema miongoni mwa watu hao, 12 walikuwa ni watoto na watu wazima ni watatu.

Misime amesema vifo hivyo vimetokea kati ya Aprili Mosi hadi Aprili 07, 2024 katika mikoa ya Rukwa, Tanga, Geita, Pwani na Mbeya ambapo baadhi ya vifo vya watu hao vilitokana na kusombwa na maji wakati wakiogelea na wengine kusababishwa na mafuriko.

Katika hatua nyingine Jeshi la Polisi limewaomba viongozi wa dini na taasisi zingine kusaidia kutoa elimu kwa watanzania na uwekaji wa alama katika maeneo hatarishi.

Chapisha Maoni

0 Maoni