Mtangazaji wa Clouds FM Gardner G. Habash afariki dunia

 

Mtangazaji nguli wa Redio ya Clouds FM, Gardner G. Habash amefariki dunia leo Aprili 20, 2024 katika Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete (JKCI) Dar es Salaam, akiwa na umri wa miaka 51.

Taarifa zilizopatikana zimesema Gadner maarufu kwa jina la 'Captain' alikuwa amelazwa JKCI akipatiwa matibabu akisumbuliwa na tatizo la shinikizo la damu (pressure).

Gardner alijipatia umaarufu mkubwa kupitia kipindi cha Jahazi cha Clouds FM, akiwa na mtangazaji mwenzake mashuhuri na rafiki yake marehemu Ephraim Kibonde.

Kutokana na ukaribu wa watangazaji hao wawili, wakati wa kifo cha Kibonde, Gadner alisema kwamba hajui atafanyakazi vipi bila ya Kibonde.

Tangulia Garnder kamsalimie rafiki yako na pacha wako katika utangazaji Ephraim Kibonde, tutaendelea kuzi-miss stori zenu na ucheshe wenu.

Chapisha Maoni

0 Maoni