Mke wa Rais wa Zanzibar, Msarifu na Mwenyekiti wa Bodi ya
wadhamini ya Taasisi ya Zanzibar Maisha Bora Foundation (ZMBF) Mhe.Mama Mariam
Mwinyi amesema Serikali itaendelea kutambua na kuthamini mchango wa Wanawake na
kuwashirikisha katika ngazi ya maamuzi na kuendeleza maendeleo nchini.
Mama Mariam Mwinyi amesema hayo katika hafla ya Uwezeshaji
na Ushirikishwaji Wanawake kiuchumi kwa Zanzibar kupitia program ya Mwanamke
Shujaa ilioandaliwa na kampuni ya Coca Cola Kwanza kwa kushirikiana na Oryx Gas
Tanzania, Shirika la Utangazaji Zanzibar (ZBC) na Wakala wa Uwezeshaji wananchi
kiuchumi Zanzibar (ZEEA) katika viwanja vya Maisara, Mkoa wa Mjini Magharibi
tarehe 20 Aprili 2024.
Aidha Mama Mariam Mwinyi ameeleza kuwa Serikali inayoongozwa
na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa
Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi inatambua na kuenzi mchango
mkubwa unaofanywa na wajasiriamali Wanawake ikiwemo Mamalishe ambao ni kundi
kubwa la Wanawake waliojiajiri kutoa
huduma ya vyakula nchini.
Mama Mariam Mwinyi ametoa rai kwa mashirika na asasi
mbalimbali za kiraia kuendeleza utaratibu wa ushirikishwaji na uwezeshaji
Wanawake kiuchumi katika kufikia malengo ya maendeleo ya jamii .
Kwa upande mwingine Mama Mariam Mwinyi amekabidhi majiko ya gesi 450 na mitungi yake, meza za majiko 450, kreti za soda 450 pamoja na Apron zaidi 1350 msaada uliotolewa na Kampuni ya Coca-Cola kwanza ikishirikiana na wadau wengine wa maendeleo wakiwemo Kampuni ya Oryx Energies , Shirika la Utangazaji Zanzibar (ZBC) pamoja na Wakala wa Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi (ZEEA).
0 Maoni