Matokeo ya Sensa ya Wanyamapori kuwekwa hadharani kesho

 

Serikali ya Tanzania kupitia Wizara ya Maliasili na Utalii inatarajiwa kesho tarehe 22.04. 2024 kutangaza rasmi matokeo ya sensa ya wanyamapori, pamoja na kuzindua ripoti ya Watalii wa Kimataifa walioitembelea nchini kwa mwaka 2023.

Utangazaji na uzinduzi huu huo utajumuisha wadau mbalimbali wa uhifadhi na utalii utafanyika katika Hoteli ya Gran Melia Jijini Arusha, ambapo Waziri wa maliasili na utalii Angellah Kairuki ndiye anayetarajiwa kutangaza matokeo hayo ya sensa na kuzindua ripoti hiyo.

Katika mkutano wake na wanahabari jijini Arusha, Mwakilishi wa Wizara ya Maliasili  na  Utalii  Dkt. Edward  Kohi  ambaye ni Mkurugenzi  wa Utafiti  na Mafunzo  amesema taarifa hizo zenye  tija katika uhifadhi wa wanyamapori na kukuza  utalii nchini  zinaakisi juhudi za Serekali  kuhifadhi  utajiri  wa Maliasili ya Wanyamapori na kukuza utalii nchini.

Aidha, ripoti hiyo itaangazia matokeo watalii walioitembelea nchi hii mwaka 2023 baada ya Rais Samia  Suluhu  Hassan  kuitangaza Tanzania  kimataifa kupitia filamu ya Royal  Tour.



Chapisha Maoni

0 Maoni