Waziri Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa amewasili leo Halmashauri
ya Mlimba, Wilaya ya Kilombero Mkoani Morogoro ambapo atakagua athari
zilizosababishwa na mafuriko yaliyotokana na mvua kubwa zinazoendelea kunyesha
nchini katika maeneo ya Taweta, Masagati, Utengule na Malinyi.
Pia Mheshimiwa Majaliwa atazungumza na wananchi waliothirika
na mafuriko hayo.
Aidha, Mheshimiwa Majaliwa pia ataelekea Wilaya ya Rufiji mkoa wa Pwani ambapo pia atakagua athari za mafuriko pamoja na kuzungumza na wananchi katika maeneo ya Muhoro na Chimbi.
0 Maoni