Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Mamlaka ya Hifadhi ya
Ngorongoro (NCAA) Jenerali Venance Mabeyo (Mstaafu) tarehe 29 Aprili, 2024
amewavisha vyeo maafisa Uhifadhi wakuu waliopandishwa vyeo hivi karibuni katika
tukio lililofanyika ofisi za Makao makuu ya NCAA Karatu Mkoani Arusha.
Waliovishwa vyeo ni Afisa Uhifadhi Mkuu Lilian Magoma ambae
amepandishwa na kuvishwa cheo kuwa Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Uhifadhi
anayesimamia idara ya Mipango, tathmini na ufuatiliajI na Afisa Uhifadhi
Mwandamizi wa Rasilimali watu Salma Chisonga aliyepandishwa cheo amevishwa cheo kuwa Kamishna msaidizi
Mwandamizi wa uhifadhi, Rasilimali watu na Utawala.
Jenerali Mabeyo amewataka makamishna wapya kufanya kazi kwa kujituma na kuzingatia viapo vyao katika misingi ya uzalendo, maadili ya utumishi, ushirikiano, maarifa na bidii ya kazi katika utekelezaji wa majukumu yao ya kila siku.
0 Maoni