Katika kuelekea Siku ya Afya Duniani Mkuu wa Wilaya ya Mvomero Mkoani Morogoro Mhe. Judith Nguli ametoa wito kwa Wakazi wa Wilaya hiyo kuhudhuria katika mabanda ya Wizara ya Afya kupata elimu ya afya na kupima afya zao.
Mhe. Nguli amesema hayo Ofisini kwake wakati akizungumza na
Elimu ya Afya kwa Umma kuelekea
Maadhimisho ya Siku ya Afya Duniani yanayokwenda sambamba na kaulimbiu isemayo
"Afya Yangu, Haki Yangu" ambapo Kitaifa yanafanyika Wilayani Mvomero
Mkoani Morogoro tangu Aprili 4-7, 2024.
Amebainisha kuwa baadhi ya maeneo ya Wilaya hiyo ikiwemo
Dakawa na Turiani ni muhimu kuchukua tahadhari.
"Kupitia Maonesho kuelekea Siku ya Afya Duniani, ambapo
yanafanyika CCM Kialawa niwasihi wananchi kupitia maonesho hayo tukapate Elimu
ya Afya maana Wizara ya Afya imefanya jambo kubwa kutusogezea huduma tena bure,"
amesema.
Hivyo, Mkuu huyo wa Wilaya amesema katika kujikinga na
Ugonjwa wa Kipindupindu ni muhimu kula
vyakula vya moto, kuchemsha maji, kuacha kufungulia majitaka ovyo,kunawa
mikono, kuosha matunda kabla ya kula.
Halikadhalika Mkuu huyo wa Wilaya amehimiza umuhimu wa
kufuata mtindo bora wa maisha ikiwemo kufanya mazoezi mara kwa mara, kuzingatia
mlo sahihi.
Na. Elimu ya Afya kwa Umma
0 Maoni