TANAPA yashinda Tuzo ya Mawasiliano ya Umma

 

Shirika la Hifadhi za Taifa Tanzania (TANAPA) kupitia Idara ya Mawasiliano imeshinda Tuzo ya Umahiri katika Mawasiliano ya Umma iliyobeba dhima ya “The Best use of Influencers Category for the year 2023”.

Hafla ya utoaji wa tuzo hiyo ilifanyika usiku wa jana tarehe 05.04.2024 katika Ukumbi wa St. Peter’s jijini Dar es Salaam, tuzo ambazo zimetolewa  na taasisi ya Public Relations Society of Tanzania (PRST).

Mgeni rasmi katika utoaji wa tuzo hiyo alikuwa Naibu Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Mhe. Mhandisi Maryprisca Winfred Mahundi.

Ushindi huo umetokana na mchango mkubwa unaotolewa na Idara ya Mawasiliano ya TANAPA katika kuhabarisha umma masuala mbalimbali ya Uhifadhi na Utalii.



Chapisha Maoni

0 Maoni