CCM inaendelea kuwachuja viongozi wake- Dkt. Nchimbi

 

Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Dkt. Emmanuel Nchimbi amesema kwamba CCM itandelea kuwachuja viongozi wake bila haya ili kuhakikisha wale ambao hawana moyo wa utumishi hawatapata nafasi ya kutumikia katika chama.

Dkt. Nchimbi amesema kiongozi wa CCM anapimwa kwa uwezo wake wa kutumikia watu, kiongozi wa chama hicho hapimwi kwa uwezo wake wa kujinufaisha binafsi, hapimwi kwa uwezo wa kunufaisha familia yake, anapimwa kwa uwezo wa kutumikia watu.

"Kadri tunavyokwenda tunaendelea kuchuja viongozi wetu na tutakuwa tunawachuja bila haya, wale ambao hawana moyo wa utumishi hawatapata nafasi ya kutumikia katika chama chetu,” amesema Dkt. Nchimbi.

Dkt. Nchimbi amesema hayo akizungumza kwenye mkutano wa hadhara uliyofanyika jana Namanyere, Nkasi, Mkoani wa Rukwa na kuongeza kuwa, “Sisi kama CCM tutakacho kitekeleza kwa nguvu zetu zote ni kuhakikisha kwamba serikali zetu wakati wote zinajielekeza katika kutumikia wananchi, hatutasita kukosoa, hatutasita kuelekeza lakini wote tukijikita katika kufanikisha maendeleo ya nchi yetu.”



Chapisha Maoni

0 Maoni