Waziri Ummy kuzishukia Hospitali za binafsi zitakazowazuia wagonjwa wa dharura

 

Waziri wa Afya Mhe. Ummy Mwalimu amezitaka hospitali za binafsi zilizogomea kitita kipya cha matibabu cha wanachama NIHF kuzingatia sheria na miongozo ya matibabu kwa kutowazuia kupata matibabu wagonjwa wa dharura.

Aidha, Mhe. Ummy amezitaka hospitali za binafsi ambazo zimegomea kitita hicho kutowaondoa wodini wagonjwa waliolazwa wanachama wa NHIF, kwa sababu kufanya hivyo ni kuvunja sheria ya madaktari sura namba 152.

Mhe. Ummy amevielekeza hospitali ama vituo vyote binafsi za umma nchini kuendelea kuwapokea wagonjwa wa dharura pindi wanapofika katika vituo vyao kwa kuwa hilo ni takwa la sheria namba 151 ya usajili wa vituo binafsi vya afya na kanuni yake namba 32.

“Kutowapokea wagonjwa wa dharua ni kuvunja sheria, nimeona matangazo ya hospitali yakisema hawatowapokea wagonjwa wanachama wa NHIF, warekebishe matangazo yao hawana utashi wa kusema hawatowapokea wagonjwa wa dharura,” alisema Mhe. Ummy.

Mhe. Ummy ametaka maelekezo yake yasimamiwe na kusema hata kama mgonjwa hana hela ili mradi tu ni mgonjwa wa dharura hapaswi kurudishwa nyumbani, mgonjwa anapaswa kwanza kupewa huduma bila kujali lolote.

“Amewataka wamiliki wa hospitali binafsi wakumbuke kuwa leseni zao zinatolewa na Wizara ya Afya, hivyo basi hawata mvumilia mtoa huduma yeyote atakayekiuka sheria na taratibu za kutoa huduma kwa watanzania, kwa hiyo warekebishe matangazo yao,” amesisitiza Mhe. Ummy.

Pia, amezitaka hospitali za Serikali,vkujiandaa vyema na kuweka utaratibu mzuri wa kupokea wagonjwa wengi zaidi ambao wanaweza kushindwa kupata huduma katika vituo binafsi huku akisisitiza umuhimu wa kuhakikisha kuwa kila mwananchi anapata huduma bora za afya kulingana na haki yake.


Chapisha Maoni

0 Maoni