TAARIFA KWA UMMA KUHUSU RATIBA YA MAZISHI YA KITAIFA YA RAIS MSTAAFU WA AWAMU YA PILI WA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA HAYATI ALHAJI ALI HASSAN MWINYI
Ndugu Wananchi na Watanzania wenzangu;
Kama tulivyojulishwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania, Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan, kwamba Rais Mstaafu wa Jamhuri
ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Ali Hassan Mwinyi, amefariki jana tarehe 29
Februari, 2024 saa 11.30 Jioni katika Hospitali ya Mzena,
kwa masikitiko makubwa, ninaomba kuungana na Mheshimiwa Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kutoa Salamu za Pole kwa Mheshimiwa Dr
Hussein Ali Hassan Mwinyi Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la
Mapinduzi, wanafamilia na Watanzania wote kwa msiba huu mkubwa wa kiongozi wetu
mpendwa.
Ndugu Wananchi na Watanzania wenzangu;
Kufuatia msiba huu, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,
ametangaza maombolezo ya siku saba na bendera kupeperushwa nusu mlingoti
kuanzia leo tarehe 1 Machi, 2024. Katika kipindi hiki cha siku saba za
maombolezo, Taifa litaungana kwa pamoja na wanafamilia katika maombolezo na
mazishi ya Kitaifa yatakayofanyika huko Unguja Zanzibar kwa ratiba ifuatayo;.
1. Ijumaa
tarehe 01 Machi, 2024;
i. Saa
3:00 Asubuhi;
Milango ya uwanja wa Uhuru itakuwa wazi kwa ajili ya
Wananchi kuingia kwa ajili ya maombolezo.
ii. Kuanzia
Saa 4:00 Asubuhi;
Viongozi mbalimbali kuwasili uwanja wa Uhuru kwa ajili ya
Maombolezo ya Kitaifa na Kuaga mwili wa Hayati Ali Hassan Mwinyi
iii. Kuanzia
Saa 5:30 Asubuhi;
Mwili wa Hayati Mzee wetu Ali Hassan Mwinyi kuondoka
nyumbani Mikocheni kuelekea Msikiti Mkuu wa BAKWATA uliopo Kinondoni ambako
Sheikh Dokta Abubakar Bin Zuber Bin Ali ataongoza swala ya Ijumaa pamoja na
taratibu zote za kidini.
iv. Saa 8:00
Mchana;
Mwili wa Hayati Ali Hassan Mwinyi kuelekea Uwanja wa Uhuru.
v. Kuanzia
Saa 8:30 Mchana;
• Dua na
maombi kutoka kwa viongozi wa dini
• Salamu
za rambirambi kutoka kwa viongozi mbalimbali;
• Viongozi
na Wananchi mbalimbali kutoa heshima za mwisho
vi. Saa 11:00
Jioni;
Mwili wa Hayati Ali Hassan Mwinyi, kuondoka uwanja wa Uhuru
kuelekea uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Julius Kambarage Nyerere;
vii. Saa 11:30
Jioni;
Wananchi wa Jiji la
Zanzibar na maeneo mengine ya Unguja kupokea Mwili wa Hayati Ali Hassan Mwinyi,
katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Abeid Aman Karume na kuelekea nyumbani
kwa marehemu.
2. Jumamosi
tarehe 02 Machi, 2024;
i. Saa
12:00 Asubuhi;
Milango ya uwanja wa Amani itakuwa wazi kuanzia saa 12:00
asubuhi ambako Shughuli ya kitaifa itafanyika.
ii. Kuanzia
Saa 3:00 Asubuhi;
Viongozi mbalimbali kuwasili uwanja wa Aman kwa ajili ya
Maombolezo ya Kitaifa na Kuaga mwili wa Hayati Ali Hassan Mwinyi
iii. Kuanzia
Saa 4:00 Asubuhi;
Mwili wa Hayati Ali Hassan Mwinyi kuondoka nyumbani kwa
marehemu kuelekea Uwanja wa Aman.
iv. Kuanzia
Saa 5:00 Mchana;
Dua na swala kutoka kwa viongozi wa dini
v. Saa 5:30
Asubuhi
• Salamu za
rambirambi kutoka kwa viongozi mbalimbali
• Salamu za
Pole kutoka kwa Mheshimiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
vi. Saa 6:30
Mchana
Viongozi na Wananchi mbalimbali kutoa heshima za mwisho
vii. Saa 9:00
Alasiri
Mwili wa Hayati Ali Hassan Mwinyi uwanja wa Aman kuelekea kijijini
kwa marehemu Mangapwani kwa ajili ya mazishi ya Kitaifa
viii. Saa 10:00
Mchana
Wananchi na Viongozi mbalimbali kushiriki Mazishi ya Kitaifa
ya hayati Ali Hassan Mwinyi eneo la Mangapwani.
Ndugu Wananchi na Watanzania wenzangu;
Watanzania tumepokea taarifa za msiba wa mzee wetu, kiongozi
wetu Rais Mstaafu wa awamu ya Pili wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa
masikitiko makubwa na Mheshimiwa Rais
Dkt. Samia Suluhu Hassan, ametutaka Watanzania wote kuwa watulivu na
wastahimilivu kutokana na kifo cha mpendwa wetu.
Ndugu Wananchi na watanzania wenzangu; pamoja na taarifa
hii, Serikali itaendelea kutoa taarifa kwa umma kuhusu matukio ya kila hatua
kupitia Msemaji Mkuu wa Serikali.
INNA LILAHI WA INNA ILAYHI RAJI’ UN
SISI SOTE NI WA MWENYEZI MUNGU NA KWAKE TUTAREJEA
CHANZO: Ofisi ya Waziri Mkuu
0 Maoni