Ubakaji kumpeleka Robinho jela miaka tisa

 

Mchezaji wa Brazil aliyewahi kuichezea Manchester City na Real Madrid, Robinho analazimika kutumikia kifungo cha miaka tisa jela kwa ubakaji nchini Brazil.

Robinho, 40, alitiwa hatiani na Mahakama ya Italia mwaka 2017 kwa kushiriki na wenzake kumbaka mwanamke mwenye miaka 22 raia wa Abainia.

Hapo jana, Majaji katika Jiji la Brasilia walisema kuwa Robinho anapaswa kutumikia kifungo hicho nchini Brazil, kufuatia maombi ya Italia.

Hata hivyo, Robinho ataendelea kuwa huru kufuatia rufaa aliyoikata dhidi ya hukumu hiyo, Wakili wake amesema.

Mchezaji huyo wa zamani wa kimataifa wa Brazil, aliyelichezea taifa lake michezo 100, wakati wa tukio hilo alikuwa anaichezea AC Milan.

Baada ya kutia hatiani alishindwa rufaa yake mwaka 2020, na kisha Mahakama ya Juu ya Italia ikakazia hukumu yake mwaka 2022.

Baada ya kushindwa rufaa waendesha mashataka wa Italia, walitoa hati ya kimataifa ya kukamatwa kwa Robinho.

Robinho, ambaye aliichezea Manchester City kwa muda wa miaka miwili, Jumapili alikiambia chomba cha habari cha Brazil kwamba kulikuwa na makubaliano ya kufanya ngono.


Chapisha Maoni

0 Maoni