Kamishna wa Uhifadhi Shirika la Hifadhi za Taifa (TANAPA),
Musa Kuji amesema katika kipindi cha miaka mitatu ya Serikali ya Awamu ya Sita ya
Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan, kumekuwepo na ongezeko la mapato kutoka shilingi
174,715,158,494 (2021/2022) hadi kufikia shilingi 337,424,076,896 (2022/2023)
sawa na ongezeko la shilingi 162,708,918,402 ambayo ni asilimia 94%.
Kamishna Kuji, ameyasema hayo leo Machi 21, 2024 Jijini Dar es
Salaam kwenye kikao kazi baina ya TANAPA na Wahariri wa vyombo vya habari chini
ya uratibu wa Ofisi ya Msajili wa Hazina ili kueleza mafanikio ya utekelezaji
wa shughuli za TANAPA katika kipindi cha miaka mitatu ya serikali ya awamu ya
sita.
Aidha, Kamishna Kuji amesema kwa mwaka wa fedha 2023/2024
(Julai 2023 hadi Machi 19, 2024) Shirika limekusanya shilingi 340,101,108,465
ukilinganisha na matarajio ya kukusanya shilingi 295,466,811,506 hadi Machi
2024.
“Kiasi hiki cha shilingi bilioni 340 ni ongezeko la shilingi
44,634,296,959 ambazo ni sawa na asilimia 15. Shirika lina matarajio ya
kukusanya kiasi cha shilingi 382,307,977,497 hadi Juni 2024,” ameelezea Kamishna
Kuji.
Pamoja na mambo mengine Kamishna Kuji amesema idadi ya
watalii wanaotarajiwa kutembelea Hifadhi za Taifa kwa mwaka wa fedha 2023/2024
ni 1,830,081 (watalii wa nje 963,413 na watalii wa ndani 866,667).
0 Maoni