Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu
Hassan, akizungumza jambo na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la
Mapinduzi Dkt. Hussein Ali Mwinyi wakati wa Hafla ya kutoa Heshima za mwisho
kwa Rais Mstaafu wa awamu ya pili Hayati Mzee Ali Hassan Mwinyi katika uwanja
wa Michezo wa Amani mjini Zanzibar. Hayati Mzee Mwinyi alifariki dunia tarehe
29 Februari 2024 katika Hospitali ya Mzena Jijini Dar es salaam alipokuwa
amelazwa akipata matibabu ya Saratani ya Mapafu, na anatarajiwa kuzikwa Kijijini
kwake Mangapwani Mkoa wa Kaskazini Unguja tarehe 02 Machi 2024.
Wajane wa Hayati Rais Mstaafu awamu ya pili Mzee Ali Hassan
Mwinyi Bibi Siti Mwinyi na Khadija Mwinyi wakiwasili katika Uwanja wa Michezo
wa Amani mjini Zanzibar tarehe 02 Machi
2024.
Askari wa Jeshi la Wananchi wa Tanzania JWTZ waliobeba Jeneza
lenye Mwili wa Rais Mstaafu awamu ya
pili Mzee Ali Hassan Mwinyi wakiwasili katika Uwanja wa Michezo wa Amani mjini
Zanzibar tarehe 02 Machi 2024.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu
Hassan, akiwa pamoja na Viongozi mbalimbali katika uwanja wa Michezo wa Amani
mjini Zanzibar kwa ajili ya kuongoza Viongozi na Wananchi wa Zanzibar kutoa
Heshima za mwisho kwa Rais Mstaafu wa awamu ya pili Hayati Mzee Ali Hassan
Mwinyi aliyefariki dunia tarehe 29 Februari 2024 katika Hospitali ya Mzena
Jijini Dar es salaam alipokuwa amelazwa akipata matibabu ya Saratani ya Mapafu, ambapo anatarajiwa
kuzikwa Kijijini kwake Mangapwani Mkoa wa Kaskazini Unguja tarehe 02 Machi
2024.
0 Maoni